COVID-19 (virusi vipya vya korona) – Maelezo, huduma, na nyenzo katika Jimbo la Washington

Nambari ya Simu ya COVID-19: Msaada kwa wafanyakazi, biashara, miadi ya chanjo na zaidi

Iwapo una maswali kuhusu COVID-19 au unahitaji msaada wa kupata miadi ya chanjo, tafadhali piga simu kwa 1-800-525-0127 na ubonyeze #. Watakapojibu, taja lugha yako ili upate huduma za ukalimani. Nambari hiyo ya simu iko wazi kila siku saa zake zimeorodheshwa katika tovuti ya Department of Health (katika Kiingereza pekee).

Ripoti ukiukaji wa kibiashara

Biashara zinapaswa kuchukua hatua zinazofaa za afya na usalama kwa ajili ya wafanyakazi na wateja. Iwapo unataka kuripoti ukiukaji, tafadhali piga nambari ya simu ya COVID-19 iliyo hapo juu ili kupata msaada katika lugha yako. Mtu fulani atakuuliza maswali kuhusu ukiukaji huo na kuwasilisha malalamishi kwa niaba yako. Hutahitajika kupeana jina lako au habari zako za mawasiliano ili kuwasilisha malalamishi.

Unaweza pia kuwasilisha malalamishi katika Kiingereza kwenye ukurasa wa Ripoti Ukiukaji wa COVID-19.

Tafadhali zingatia kwamba ikiwa utatoa jina lako au habari yako za mawasiliano, zinaweza kufunuliwa ikiwa mtu atawasilisha ombi la rekodi za umma kwa ajili ya habari hizo. Rekodi zinazofafanuliwa katika Taarifa ya Faragha ya gavana (katika Kiingereza pekee) zitatolewa jinsi zinavyopaswa kulingana na Sheria ya jimbo ya Rekodi za Umma, RCW 42.56.

Msaada zaidi kwa wafanyakazi, biashara na mashirika

Kwa kutumia huduma za utafsiri, nambari hio ya simu inaweza kukuelekeza kwa mwongozo wa jumla na rasilimali. Zinaweza pia kukusaidia kujaza fomu ya COVID-19 ya Maswali ya Biashara na Wafanyakazi ikiwa bado una maswali. Utaombwa kuandaa habari za mawasiliano ili uweze kupata jibu.

Chanjo ya Virusi vya Korona (COVID-19)

Kwa maelezo zaidi kuhusu chanjo za COVID-19, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa Chanjo dhidi ya COVID-19.

Programu ya simu mahiri ya arifa za kuwa katika hatari ya WA Notify

Ikiwa ungependa kujifunza mengi kuhusu WA Notify, ikijumuisha jinsi ya kuiongeza kwenye simu yako, tembelea WANotify.org

Nyenzo Zinazohusiana na Ajira na Biashara

Mafao ya Kukosa Ajira

Ikiwa umepoteza kazi, unaweza kustahiki mafao ya kukosa ajira. Ikiwa unahitaji maelezo kuhusu jinsi ya kujaza madai kwa ajili ya mafao ya kukosa ajira, unaweza kupiga simu 1-800-318-6022. Wakipokea simu, sema lugha yako ili kupata huduma za ukalimani.

Wafanyakazi na Wamiliki wa Biashara

Janga la virusi vya korona limeathiri mamia ya maelfu ya wafanyakazi na waajiri katika jimbo letu.

Ili kudumisha usalama wafanyakazi, waajiri wanapaswa:

 • Kuwaelimisha wafanyakazi wao kuhusu ishara na dalili za COVID-19 katika lugha ambayo wanaielewa.
 • Kutekeleza mpango wa kudumisha umbali wa kutengana.
 • Kufanya usafi na uuaji wa vimelea wa mara kwa mara.
 • Kuhakikisha unawaji wa mikono wa mara kwa mara na sahihi.
 • Hakikisha wafanyakazi wagonjwa wanakaa nyumbani.

Majibu kwa maswali ya kawaida kuhusu likizo inayolipwa ya ugonjwa, ufidiaji wa mfanyakazi na muhtasari wa masharti ya usalama wa mahali pa kazi zinapatikana kutoka Department of Labor & Industries (Idara ya Kazi na Viwanda) kwa lugha mbalimbali.

Ikiwa una wasiwasi juu ya usalama wa mahali pako pa kazi, unaweza kuwasilisha malalamiko kwa kuwapigia simu Department of Labor & Industries moja kwa moja kwa nambari 800-423-7233. Huduma za ukalimani kwa njia ya simu zinapatikana.

Ikiwa una maswali kuhusu biashara na wafanyakazi wako katika kipindi cha COVID19, unaweza kuwapigia simu Employment Security Department (Idara ya Usalama wa Wafanyakazi) kwa nambari 855-829-9243.

Nyezo za Huduma ya Afya na Bima ya Afya

Unaweza kustahiki bima ya afya ya bila malipo au ya gharama nafuu. Wapigie simu Health Care Authority (Mamlaka ya Huduma za Afya kwa nambari 1-855-923-4633. Wakipokea simu, sema lugha yako ili kupata huduma za ukalimani.

Bima ya Alien Emergency Medical (AEM) ni mpango kwa ajili ya watu ambao wanastahiki matibabu ya dharura ambazo hawakidhi vigezo vya uraia au uhamiaji, au ni mtu anayestahiki ambaye hajatimiza miaka 5 ya sheria.

Namba ya simu ya dharura ya Help Me Grow ya Washington 1-800-322-2588 inaweza kutambua mipango na huduma mbalimbali unazostahiki na kukusaidia kuziomba. Hii inajumuisha:

 • WIC (Mpango wa Afya wa Wanawake, Watoto wachanga & Watoto)
 • Bima ya Afya kwa watoto, wanawake wajawazito na watu wazima
 • Upangaji uzazi kupitia Mpango wa Take Charge
 • Kliniki za afya na upangaji uzazi
 • Vifaa vya ujauzito na mtoto mchanga
 • Usaidizi katika kunyonyesha
 • Pia wana mipango na nyenzo kuhusu vyakula.
Maelezo ya Wakimbizi na Wahamiaji

Office of Immigrant and Refugee Affairs (Afisi ya Mambo ya Wahamiaji na Wakimbizi) (OIRA) inawasaidia wahamiaji kuelewa maelezo muhimu kuhusu COVID-19 na kuhusu wasiwasi wa mhamiaji. Baadhi ya mambo mengine muhimu ya kuyafahamu:

 • Hospitali na kliniki haziruhusiwi kushiriki uraia au hadhi ya uhamiaji na ICE.
 • Kupimwa COVID-19 na kupata msaada au punguzo la huduma ya afya halitaathiri uwezo wako wa kuomba kadi ya kijani au uraia.
 • Unapaswa kuwa na nambari halali ya ustawi wa jamii kwa ajili ya mafao ya kukosa ajira. Ikiwa ungependa kuzungumza na mtu kuhusu namna ya kupata mafao ya kukosa ajira piga simu 1-800-318-6022.
 • Kupokea mafao ya kutokuwa na ajira hakutatishia uwezo wako wa kuomba au kadi ya kijani au uraia chini ya sheria ya Usaidizi kutoka kwa Fedha za Umma.
 • Unaweza kustahiki Likizo Yenye Malipo ya Familia na Matibabu katika Jimbo la Washington ili kumhudumia mtu ambaye anaugua Covid-19 au kujihudumia mwenyewe iwapo una virusi. Hupaswi kuwa nambari ya ustawi wa jamii ili kupata fao hili. ESD inakubali hati zingine za aina nyingi.
 • Iwapo unamiliki biashara na unatafuta usaidizi, hatua ya kutuma maombi ya mkopo kutoka kwa Federal Small Business Administration (Mamlaka ya Usaidizi wa Biashara Ndogo ya Nchi) haitaathiri uwezo wako wa kupata kadi ya mkaazi au uraia.

Office of Immigrant and Refugee Affairs (Afisi ya Mambo ya Wahamiaji na Wakimbizi) (OIRA) inapendekeza kuwa iwapo hauna uhakika kuhusu hali yako au ya mwanafamilia, au kuhusu manufaa yako, wasiliana na wakili wa uhamiaji, afisa wa uhamiaji au mwakilishi aliyeidhinishwa na Department of Justice (Idara ya Sheria) (DOJ). Unaweza kupata wakili kupitia American Immigration Lawyers Association (Shirika la Mawakili wa Uhamiaji la Marekani), au unaweza kutembelea tovuti ya shirika lililoidhinishwa na DOJ.

OIRA ina mipango ya kuwasaidia wakimbizi na wahamiaji kwa ajili ya:

 • Utafutaji wa kazi na mafunzo.
 • Usaidizi katika uhamiaji.
 • Ushauri kwa vijana.
 • Msaada kwa wakimbizi wazee, watoto, wanafunzi na wengine.
 • Mipango ya kawaida ipo wazi kwa mbali katika kipindi cha COVID-19. Ofisi ina huduma mpya za kukusaidia kuomba kazi au mafao ya kukosa ajira, kusaidia elimu yako, na kutoa usaidizi wa makazi. Ustahiki katika Msaada wa Fedha za Wakimbizi na Msaada wa Matibabu wa Wakimbizi umeongezwa hadi Sept. 30, 2020.
 • Kwa huduma na maelezo zaidi, piga simu 360-890-0691.

Kwa maswali kuhusu haki za wahamiaji, kupata usaidizi wa rufaa kwa ndugu/marafiki ambao wamewekwa kizuizini, na maelezo mengine yanayohusiana, unaweza kuwasiliana na Mtandao wa Mshikamano wa Wahamiaji wa Washington (Washington Immigrant Solidarity Network) kwa nambari 1-844-724-3737. Huduma za ukalimani kwa njia ya simu unapatikana.

Afya ya Akili na Hisia

Huu unaweza kuwa muda mgumu sana. Ni kawaida wewe au uwapendao mnaweza kuhisi wasiwasi, huzuni, hofu au hasira. Hauko peke yako. Ni sawa kutafuta na kuomba msaada.

Kila mtu anaathiriwa tofauti msongo wa mawazo na hali ngumu. Kitu cha muhimu zaidi unachoweza kukifanya ni kujijali wewe mwenyewe, familia yako, na jamii vizuri kadri uwezavyo.

Je, ni nini kinakusaidia ili ukabiliane na nyakati za changamoto? Je, unaendelea kuwasiliana na kuingiliana na marafiki na familia? Labda unazingatia kupumua kwa nguvu na kujinyoosha, mazoezi kadhaa au usiku mzuri wa kulala? Kutenga muda kwa ajili ya kujijali ni kipaumbele, hata kama hupendelei, kunaweza kusaidia kupunguza msongo wa mawazo.

Ikiwa upo kwenye mgogoro na unahitaji kuzungumza na mtu ili akupe unasihi, kuna machaguo machache.

 • Disaster Distress Helpline inatoa unasihi wa haraka wa mgogoro kwa watu wanaopitia matatizo ya kihisia yanayohusiana na majanga ya asili au yaliyosababishwa na binadamu Piga Simu 1-800-985-5990. Wakipokea simu, sema lugha yako ili kupata huduma ya ukalimani. Simu ya usaidizi inapatikana saa 24 kwa siku kila siku.
 • Crisis Connections ina Namba ya Simu ya Saa 24 ambayo inatoa usaidizi wa papo hapo kwa watu, familia na marafiki wa watu wenye tatizo la hisia. Inawahudumia watu wanaoishi Kaunti ya King. Huduma za ukalimani wa lugha zinapatikana. Piga simu 1-866-427-4747.
 • National Suicide Prevention Lifeline inatoa nyenzo za kinga na migogoro kwa watu wanaofikiria kuhusu kujiua. Wapendwa wako pia wanaweza kuwapigia simu lifelineili kupata rasilimali za kuisaidia familia na marafiki wao. Piga simu 1-800-273-8255. Namba ya simu hii inapatikana saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki. Kuna namba ya simu maalumu ya usaidizi kwa ajili ya wanajeshi wastaafu. Piga simu 1-800-273-8255 kisha bonyeza 1. Ikiwa wewe ni kipofu na una tatizo la kusikia, piga simu 1-800-799-4889.
Nyenzo za Vyakula

Ikiwa una mtoto mwenye umri wa miaka 18 au chini anaweza kupata chakula cha bure kutoka shule. Watu wazima wenye ulemavu waliojiunga katika mipango ya elimu pia wanaweza kustahiki chakula cha shule. Mara nyingi, milo hii hupelekwa au huwekwa katika maeneo ya nje ya shule kama vile vituo vya basi. Wasiliana na wilaya ya shule yako kufahamu kama wanatoa chakula cha bure.

Kwa wale wote wenye ujauzito, wamama wapya na watoto wenye umri chini ya miaka mitano, unaweza kupata chakula kupitia mpango wa Department of Health’s Women, Infants and Children (WIC). Kwa usaidizi wa lugha, piga simu 1-866-632-9992.

Huenda hifadhi za chakula zimebadlisha saa za kazi au zinaweza kuwa zimefungwa kwa watu wanaotembelea maeneo yao kwa sababu ya ongezeko la mahitaji ya chakula katika kipindi cha Covid-19. Tafadhali piga simu kabla ya kwenda. Northwest Harvest ni mtandao wa hifadhi ya chakula ya jimbo zima. Andika jina la jiji lako kwenye kisanduku katika tovuti hii.

Ikiwa unaishi Mashariki ya Washington unaweza kupata orodha ya hifadhi za chakula katika Second Harvest. Chagua kaunti yako katika tovuti hii kwa ajili ya orodha ya hifadhi za chakula katika eneo lako.

Kadi za msaada wa vyakula vya msingi

Kadi za msaada vya vyakula vya msingi (EBT) zinaweza kununua vyakula na zinapatikana kwa watu mbalimbali. Raia wa Marekani wanaweza kuomba msaada huu katika ukurasa wa Vyakula vya Msingi kwenye tovuti ya Department of Social and Health Services (DSHS) ya Jimbo la Washington.

Kumbuka: Serikanli ya nchi ilisimamisha masharti ya kuwa na kazi ambayo yalitumika kwa baadhi ya watu wazima wakati wa mgogoro huu. Hata hivyo, serikali ya nchi inahitaji uwe raia wa Marekani ili uweze kustahiki kwa msaada huu.

Kadi zinazofanana na kadi za mkopo kama zilizoelezwa hapo juu zinapatikana kwa watu wengi ambao sio raia na ambao wanakidhi masharti yote mengine ya mpango. Unaweza kuomba msaada huu kupitia State Food Assistance Program wa DSHS (kwa Kiingereza pekee).

Maelezo na Rasilimali kwa Familia

Huu ni muda mgumu sana kwa familia nzima. Hizi hapa ni dondoo kadhaa za jinsi ya kuishughulikia hali hii pamoja na watoto wako:

Fanya majadiliano na familia katika sehemu nzuri na wahimize wanafamilia kuuliza maswali. Zingatia kuwa na mijadala tofauti na watoto wadogo ili kutumia lugha ambayo wanaweza kuielewa na kushughulikia hofu zao mahsusi au imani potofu.

Ingawa unapaswa kuendelea kupata taarifa, punguza kukaa kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii ambayo inaweza kuchochea woga na hofu. Kuwa na ufahamu hasa wa (na upunguze) kiasi cha taarifa za matukio katika vyombo vya habari au muda wa mitandao ya kijamii ambao watoto wako wanafuatilia kuhusu janga hili.

Zingatia kuwasaidia watoto kwa kuwahimiza waulize maswali na kuwasaidia kuelewa hali ya sasa.

 • Zungumza kuhusu hisia zao kisha uwaonyeshe unaelewa hisia zao.
 • Wasaidie kueleza hisia zao kupitia michoro au shughuli nzingine.
 • Fafanua taarifa potofu au kutoelewana kuhusu jinsi virusi vinaenea na kwamba si kila ugonjwa wa njia ya hewa ni virusi vipya vya korona ambavyo vinaweza kusababisha COVID-19.
 • Wapatie faraja na uvumilivu wa ziada.
 • Wakague watoto wako mara kwa mara au pale hali inapobadilika.
 • Weka ratiba ya familia yako inayofanana linapokuja suala la kulala, kula na mazoezi.
 • Tenga muda wa kufanya mambo nyumbani ambayo tatakufanya wewe pamoja na familia yako mjisikie vizuri katika hali zingine ngumu, kama vile kusoma, kutazama filamu, kusikiliza muziki, kucheza michezo, au kushiriki katika shughuli za kidini (maombi, kushiriki katika huduma Intaneti).
 • Tambua kwamba hisia kama vile upweke, uchovu, hofu ya kuambukizwa ugonjwa, wasiwasi, msongo wa mawazo, na hofu ni athari za kawaida katika hali gumu kama vile ya janga.
 • Isaidie familia yako kushiriki katika shuguli za burudani na muhimu zinazoendana na maadili ya familia na utamaduni wako.
Nyenzo na Maelezo ya Ziada

Washington State Commission on Asian Pacific American Affairs (CAPAA)